Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ataka kuwepo matumizi ya nishati safi

Ban ataka kuwepo matumizi ya nishati safi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema kuwa matumizi ya nishati safi duniani ni lazima yaambatane na changamoto za kijamii, kiuchumi na za kimazingira.

Akizungumza kwenye mkutano kuhusu matumizi ya nishati safi mjini Copenhagen Ban amesema kuwa kwa sasa ulimwengu unakabiliwa na changamoto za chakula , mafuta na uchumi kwa hivyo masuala ya uchumi , mazingira na usawa vinastahili kupewa kipaumbele. Ban pia amesema kuwa matumizi ya nishati safi inaweza kusaidia kuwepo maendeleo ya karne ya 21.