Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hofu kutokana na ghasia kwenye Ukingo wa Magharibi:UM

Hofu kutokana na ghasia kwenye Ukingo wa Magharibi:UM

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeelezea wasi wasi wake kutokana na ghasia zinazoendeshwa na walowezi wa kiyahudi dhidi ya raia wa kipalestina kwenye ukingo wa magharibi tangu mwezi Septemba. Kijiji cha Qusra karibu na mji wa Nablus kaskazini kwa ukingo wa Magharibi kimekuwa kikilengwa na walowezi kwa muda wa karibu majuma sita yaliyopita.

Ofisi ya haki za binadamu ya UM inasema kuwa gahasia hizo zimesababisha uharibifu wa mali na majeraha makubwa . Rupert Colville kutoka ofisi ya haki za binadamu anaeleza.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)