Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miji ya Pakistan yajiunga kwenye mpango wa UM

Miji ya Pakistan yajiunga kwenye mpango wa UM

Zaidi ya miji 30 nchini Pakistan imejiunga kwenye mpango unaendeshwa na Umoja wa Mataifa wenye shabaha ya kupiga kampeni ya kujiandaa na majanga ya kimazingira. Mpango huo unaendeshwa na Umoja wa Mataifa ni hatua ya awali ya kuyaandaa maeneo yanayokumbwa mara kwa mara na matukio ya majanga ya kimaumbile yakijiweka sawa kwa hali yoyote inayoweza kusababishwa.

Miji hii imeweka saini ya kuafiki kushiriki kwenye mpango huo katika wakati ambapo maeneo mengi bado yameendelea kutuwama na maji kufuatia mafuriko makubwa yaliyoikumba nchi hiyo hivi karibuni. Baadhi ya majiji yalijiunga kwenye kampeni hiyo ni pamoja na Karachi, Muzaffarabad, Dadu, Ghari Khairo, Tharparkar, Nowshera na Mnagora.