Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahabusu wa vita wanateswa Afghanistan:UNAMA

Mahabusu wa vita wanateswa Afghanistan:UNAMA

Mahabusu nchini Afghanistan wanakabiliana na baadhi ya mifumo ya utesaji imesema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa.

Mpango wa msaada wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNAMA umesema hayo baada ya kuwahoji mahabusu wanaoshikiliwa kwa sababu zinazohusiana na vita ambao walikamatwa na posili au idara ya upelelezi ya nchi hiyo.

UNAMA inasema inatarajia ripoti hiyo itasaidia kuleta mabadiliko katika mfumo ma sekta ya sheria ya nchi hiyo. Georgette Gagnon mkurugenzi wa haki za binadamu wa UNAMA anasema wafungwa 400 walohojia katika mahabusu za nchi nzima ya Afghanistan na kubaini kwamba karibu nusu ya mahabusu hao wameteswa na jeshi la polisi la nchi hiyo na idara ya pelelezi.

Wengi wamejeruhiwa na kuathirika kisaikolojia kutokana na kushinikizwa kukiri au kulazimishwa kutoa taarifa kwa polisi.