Skip to main content

Thailand yatakiwa kufanyia marekebisho sheria zake za uhuru wa kujieleza

Thailand yatakiwa kufanyia marekebisho sheria zake za uhuru wa kujieleza

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya uhuru wa maoni na wa kujieleleza Frank La Rue ameitaka serikali ya Thailand kufanyia marekebisho sheria zake zinazohusu uhuru wa maoni ambazo kwa mujibu wa kifungu namba 112 cha nchi hiyo mtu yeyote anaye mdaharau, kumtukana au kumtishia mfalme, malkia au mwana mfalme ataadhibiwa kwenda jela miaka mitatu hadi 15.

Amesema anataka sheria hizo zifanyiwe marekebisho ili kwenda sambamba na wajibu wa taifa hilo wa kutimiza haki za kimataifa za binadamu. Amesema hukumu ya makosa hayo ni kali mmno na zinakiuka haki za watu kuweza kutoa maoni na kujieleza na mara nyingi kesi zinafanyika kwa faragha na washitakiwa hawapati haki ya kijitetea ipasavyo. La Rue amesema Thailand imekuwa sehemu ya mkataba wa kimataifa wa haki za kijamii na kisiasa tangu mwaka 1996 jambo ambalo linaiweka nchi hiyo katika wajibu wa kuhakikisha kila mtu anapata fursa na haki ya kutoa maoni na kujieleza.