Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utalii bora utasaidia kufikia malengo ya maendeleo ya milenia:Migiro

Utalii bora utasaidia kufikia malengo ya maendeleo ya milenia:Migiro

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha Rose Migiro amezitaka serikali, wahisani na taasisi za fedha za kimataifa kutumia uwezo wa utalii kwa ajili ya maendeleo. Migiro amesema sekta ya utalii ina uwezo mkubwa wa kutoa nafasi za ajira, kuchagiza ukuaji wa uchumi na kupunguza umasikini. Akihutubia kikao cha 19 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa la shirika la utalii UNWTO mjini Gyeongju Jamhuri ya Korea Bi Migiro amesema utalii umekuwa moja ya sekta muhimu sana za kiuchumi duniani. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)