Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umaskini wa nishati ni tishio la kufikia malengo ya milenia:Ban

Umaskini wa nishati ni tishio la kufikia malengo ya milenia:Ban

Umasikini wa nishati ni tishio kubwa la kufikia malengo yote ya maendeleo ya milenia ameonya Katibu Mkuu wa UMoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa kimataifa wa nishati mjini Oslo wenye mada “nishati kwa wote, kufadhili upatikanaji kwa nchi masikini”

Ban amesema umasikini wa nishati unadumaza ukuaji wa uchumi na upatikanaji wa ajira na suluhu muafaka ni kuhakikisha watu wote wanapata fursa ya kuwa na nishati kwa gharama nafuu. Ameongeza kuwa nishati endelevu ni muhimu sana kwa maendeleo ya binadamu, afya, elimu, usalama, ajira na ushindani wa kiuchumi.

Kwa kulitambua hilo Ban amesema ndio maana ametoa kipaumbele kwa nishati kuwa ni kitovu cha mikakati ya maendeleo. Ban amesema kwa pamoja lengo la nishati kwa wote ifikapo mwaka 2030 linaweza kufikiwa na kuhakikisha hakuna atakayesalia kizani.