Hatua zimepigwa kimaendeleo Afrika baada ya miaka 10:NEPAD

7 Oktoba 2011

 

Nchi za Afrika zimepiga hatua tangu kupitishwa kwa mpango mpya wa ushirikiano kwa ajili ya maendeleo barani Afrika NEPAD amesema afisa wa Umoja wa Mataifa.

Cheick Diarra ambaye ni mshauri maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Afrika amesema lengo kubwa la NEPAD ambayo ilianzishwa Julai mwaka 2001 ni kuisaidia Afrika katika umasikini na kutokuwa na maendeleo na kutengwa na uchumi unaozidi kungara wa utandawazi.

Akizungumza kwenye hafla ya miaka 10 iliyopewa jina NEPAD na malengo ya maendeleo ya milenia, hatua, changamoto na mustakhabali, tangu kuanzishwa kwa NEPAD Rais wa Baraza Kuu la 66 la Umoja wa Mataifa Abdulaziz Al-Nasser amesema Afrika ni maskani ya uchumi 6 kati ya kumi zinazokuwa kwa kasi duniani hivi sasa, na ukuaji huo unavutia uwekezaji wa moja kwa moja. Sekta za jamii kama afya na elimu pia zimepiga hatua kubwa ikilinganishwa na miaka 10 iliyopita

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter