Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utafiti zaidi utahitajika kukabilia NCD's Afrika

Utafiti zaidi utahitajika kukabilia NCD's Afrika

Maradhi ya kisukari, moyo, saratani na matatizo ya kupumua kwa miaka mingi yamekuwa yakizikumba zaidi nchi zilizoendelea na ndio maana hata kuna baadhi ya nchi waliyachukulia kama ni magonjwa ya matajiri, lakini mtazamo umebadilika.

Mkutano wa wakuu wa nchi kwenye Umoja wa Mataifa mwezi uliopita kwenye mjadala wa Baraza Kuu la 66 ulifahamishwa kwamba magonjwa haya sasa yameingia katika nchi zinazoendelea na nyingi ni masikini hata kumudu matibabu na gharama zake.

Nchi mbalimbali zimeanza kuweka mikakati ya kitaifa na kuchukua hatua mbalimbali za kuelimisha jamii kuhusu njia za kujikinga, kukabiliana na maradhi hayo, pa kupata msaada na taarifa, lakini si jambo rahisi lina changamoto nyingi ikiwemo fedha.

Mbali ya hayo utafiti wa kina unahitajika kwa mataifa masikini kutambua ukubwa wa tatizo ili kurahisisha mipango ya kulishughulikia. Tanzania ni moja ya mataifa hayo na waziri wake wa Afya ni mheshimiwa Haji Mponda katika sehemu hii ya pili ya majadala na Flora Nducha anafafanua kuhusu changamoto hizo.

(MAHOJIANO NA MPONDA2)