Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR na Rwanda wajadili hatma ya wakimbizi

UNHCR na Rwanda wajadili hatma ya wakimbizi

Serikali ya Rwanda na kamishina mkuu wa shirika la Umoja wa mataifa la wakimbizi UNHCR wamektana mjini Geneva kujadili hatua zilizopigwa kupata sukluhu ya wakimbizi wa Rwanda.

Pande hizo mbili zilikwa kwenye kikao cha 62 kamati kuu ya UNHCR zimesema bado zimejidhatiti kupiga hatua ya suluhu ya wakimbizi na kuuafikiana kwamba mkutano wa pande zote husika utafanyika Desemba mwaka huu kwa mtazamo wa kshwishi wakimbizi kurejea nyumbani kwa hiyari, kwapa fursa ya kuanza maisha mapya au kupewa hadhi za kuishi kisheria katika nchi wanazoomba hifadhi.

Kusitisha hadhi ya ukimbizi ni moja ya vipengee katika mkakati huo na kwa maana hii UNHCR itapendekeza kwa mataifa kupitisha sheria ya kusitisha hadhi ya kimbizi ifikapo Desemba 31 mwaka 2011 na kuanza ktekelezwa rasmi Juni 30 mwaka 2012 ili kuchapuza mchakato wa suluhu ya wakimbizi wa Rwanda na kumudu utekelezaji wa usitishaji wa hadhi hizo kwa njia inayostahili na itakayowalinda wakimbizi hao.