Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuzo ya amani ya Nobel yaenda kwa wanawake watatu wanaharakati wa haki za binadamu

Tuzo ya amani ya Nobel yaenda kwa wanawake watatu wanaharakati wa haki za binadamu

Mwanamke wa kwanza kuchagulia kuwa Rais barani Afrika, mwanaharakati wa kupinga ubakaji Liberia na mwanamke wa Yemen aliyesimama kidete dhidi ya utawala wa nchi hiyo ndio washindi wa tuzo ya amani ya Nobel ya mwaka huu iliyotangazwa mapema leo asubuhi.

Wanawake hao watatu Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf, mwanaharakati wa haki za binadamu Leyma Gbowee wa Liberia na mwanaharakati wa kupigania demokrasia Yemen Tawakkul Karma ambaye ni mwanamke wa kwanza kushinda tuzo ya amani kwenye ulimwengu wa Kiarabu, wameshinda tuzo hii kwa kutambua umuhimu wa haki za wanawake wa kutangaza ujumbe wa amani duniani.

Tuzo hiyo inayoambatana na dola milioni 1.5 itagawanywa sawia kwa wanawake hao watatu. Akizungumzia washindi wa tuzo hiyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema hii ni habari njema na imekwenda kwa watu muafaka.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)