Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana waueleza UM hofu yao kuhusu athari za matatizo ya kiuchumi

Vijana waueleza UM hofu yao kuhusu athari za matatizo ya kiuchumi

Vijana kutoka mataifa 22 wanakutana kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa wiki hii ili kutanabaisha athari za mdororo wa kiamatifa wa uchumi kwa vijana duniani kote.

Ukosefu wa ajira, kupunguza kwa ufadhili wa elimu na haja ya kuwahusisha vijana katika maamuzi ni miongoni mwa masuala ambayo ujumbe wa vijana hao wamekwa wakiwasilisha kwa viongozi mbalimbali wa Umoja wa Mataifa kuanzia walipowasili mwanzoni mwa wiki.

Vijana hao ambao watakuwa hapa kwa wiki mbili tayari wameshakutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na kujadili naye masuala yanayowasumbua na kupendekeza suluhisho. Vijana hao wamesema sintofahamu ya hatima yao katika soko la ajira na vikwazo vinavyowakabili vijana wengi wenye taalumu ni changamoto kubwa katika nchi wanazotoka.

Katika ajira wamesema kupata kazi ni shida na kupata ajira ambayo wameisomea ni ngumu zaidi. Wakizungumza katika kamati ya tatu ya Baraza Kuu inayohusika na masuala ya uchumi wamesema bei za nyumba ni kubwa sana na vijana wengi hawataweza kumudu kumiliki nyumba hizo.