Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban asikitishwa na Baraza la Usalama kutoafikiana kuhusu Syria

Ban asikitishwa na Baraza la Usalama kutoafikiana kuhusu Syria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema amesikitishwa na kitendo cha Baraza la Usalama kushindwa kuafikiana kuhusu azimio dhidi ya Syria.

Jumanne siku Uchina na Urusi walipiga kura ya turufu kupinga azimio linalotishia kuiwekea vikwazo Syria endapo haitositisha mashambulizi ya kijeshi dhiri ya raia wanaoandamana kwa amani. Wajumbe wengine wane wa baraza hilo hawakupiga kura.

Martin Nesirky msemaji wa Umoja wa Mataifa anasema Katibu Mkuu anaamini kwamba ghasia zinazoendelea Syria hazikubaliki.

(SAUTI YA MARTIN NESIRKY)