Afisa wa UM atembelea Pakistan kukagua mkwamo uliosababishwa na mafuriko

6 Oktoba 2011

Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalojihusisha na upunguzaji majanga kwenye maeneo yaliyokumbwa na matukio mabaya, amewasili nchini Pakistan ambako anatazamiwa kukutana na maafisa wa serikali kwa ajili ya kujadilia hatua za dharura zitakazosaidia kupunguza mkwamo uliosababishwa na mafuriko ambayo yameharibu mfumo mzima wan chi hiyo.

Bi Margareta Wahlström,akiwa nchini humo anatazamiwa kukutana na mwenyeji wake rais Asif Ali Zardari ambako watajaliana kwa kina juu ya hatua za haraka kuchukuliwa ili kufupisha athari za mafuriko hayo. Kandoni mwa hayo pia anatazamiwa kukutana na waziri mkuu Syed Yusuf Raza Gilani na maafisa waandamizi wa serikali wakizingatia agenda hiyo hiyo moja.

Ziara yake hii ya siku tatu pia itamchukua hadi kwa maafisa wa mambo ya hali ya hewa na wataalamu wa kusimamia matatizo yaletwayo na majanga ya kimaumbile. Katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita, taifa la Pakistan limeshuhudia mkwamo mkubwa huku maeneo yake mengi yakisambaratishwa vibaya kutokana na mafuriko.Mamia ya watu wamepoteza maisha huku wengine wakiyapoteza makazi yao.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter