5 Oktoba 2011
Umoja wa Mataifa umeipongeza Mexico ambayo hivi karibuni imetangaza kuchukua hatua madhubiti za kuwanusuru raia wake kutoka kwenye majanga ya kimaumbile kama tetemeko la ardhi. Kupitia sheria yake mpya, serikali imeridhia kutoa uangalizi wa karibu pamoja na kutoa hifadhi salama za nyumba wakati kunapojiri matukio kama tetemeko la ardhi.
Wiki iliyopita serikali hiyo ilipitisha sheria mpya inayoweka zingatia la usalama zaidi wakati kunajiri tetemeko la ardhi. Sheria hiyo mpya imepitishwa katika wakati ambapo kukifanyika maadhimisho 26 ambayo yanatoa kumbukumbua ya tetemeko la ardhi baya kuwahi kushuhudia lililojiri mnamo septemba 1985 na kupoteza maisha ya watu 9,500 na kuharibu mfumo wa makazi.