Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taifa changa kabisa duniani Sudan Kusini lajiunga na ITU

Taifa changa kabisa duniani Sudan Kusini lajiunga na ITU

Muungano wa kimataifa wa mawasiliano ITU umesema unafuraha kubwa kutangaza kwamba taifa changa kabisa duniani Sudan Kusini limejiunga na ITU na kuwa taifa mwanachama wa 193 kuanzia Oktoba 3 mwaka huu.

Taifa hilo ambalo limejinyakulia uhuru wake Julai 9 mwaka 2011 tayari limeshapewa namba ya kimataifa ya nchi hiyo ambayo ni +211, baada ya nchi hiyo kutambuliwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Namba hiyo imeanza kutumika rasmi Septemba 28. Jason Nyakundi anaarifu.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)