Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF na washirika wajadili mahitaji ya lishe

UNICEF na washirika wajadili mahitaji ya lishe

Shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limewaleta pamoja takriban washirika 100 kujadili kuendendelea kuongezeka kwa mahitaji ya bidhaa za lishe na kutoa wito wa kuwepo ushirikiano miongoni mwa mashirika ya Umoja wa Mataifa, mashirika ya umma, wasomi na sekta ya lishe.

UNICEF huwa inachukua asilimia 80 ya chakula kilicho tayari kutumika duniani kinachopewa watoto waliokumbwa na hali mbaya ya utapiamlo walio chini ya miaka mitano.