Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yazindua mpango wa kusaidia jamii za wafugaji

IOM yazindua mpango wa kusaidia jamii za wafugaji

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limeendesha shughuli ya kununua mifugo kutoka kwa jamii ya Kulan Kaskazini mwa Kenya ambapo wafugaji 1000 katika eneo hilo walifaidika na zoezi hili. IOM ina lengo la kuisaidia jamii hiyo kuepukana na athari za ukame katika eneo hilo na hatari inayokodolea macho mifugo wao. Jamii za wafugaji zimeathirika na athari za ukame na pia zinakumbwa na hatari ya kupoteza mifugo wao kutokana na magonjwa, njaa na kiu zinapojaribu kuwatafutia mifugo wao malisho na maji. George Njogopa anaripoti