Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maelfu wahama makwao kutokana na mashambulizi kaskazini mwa Iraq

Maelfu wahama makwao kutokana na mashambulizi kaskazini mwa Iraq

Takriban wakimbizi 600 wamepokea usaidizi kutoka kwa kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu ICRC kaskakazini mwa Iraq. Familia hizo ni miongoni mwa wale waliohama makwao kutokana na kuwepo mashambulizi ya mabomu ambayo yamekuwa yakiendelea katika eneo hilo tangu miiezi mitatu iliyopita. Familia hizo 98 kutoka vijiji 98 kutoka eneo la Kurdistan ziliwasili kwenye wilaya ya Soran majuma kadha yaliyopita baada ya kukimbia na kuacha kilicho chao nyuma na kwa sasa wanaishi chini ya mahema wakikabiliwa na ukosefu wa maji ya kunywa na umeme. Tangu kuanza kwa mashambulizi hayo mwezi Julai ICRC imekuwa ikitoa misaada ya kibinadamu kwa zaidi ya watu 2500 waliolazimika kuhama makwao kutokana na mashambulizi hayo.