Ofisi ya haki za binadamu ya UM yalaani maandamano nchini Bulgaria

4 Oktoba 2011

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeelezea hisia zake kufuatia maandamano ya kupinga jamii ya Roma nchini Bulgaria baada ya kijana mmoja kuuawa alipogongwa na gari inayomilikiwa na mtu kutoka jamii hiyo. 

Maandamano hayo yaliyoanza Septemba 23 yamesambaa kwenda miji mingine. Ofisi ya haki za binadamu ya UM inasema kuwa inajutia kifo cha kijana huyo na kutaka dereva wa gari hilo kufikishwa mbele ya sheria ili ukweli kuhusu kifo hicho uweze kubainika. Rupert Colville kutoka ofisi ya haki za binadamu ya UM anaeleza. 

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud