Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usalama mdogo, na barabara mbaya ni adha kwa wakimbizi Sudan Kusini

Usalama mdogo, na barabara mbaya ni adha kwa wakimbizi Sudan Kusini

Wafanyikazi wa kutoa huduma za matababu kutoka shirika la kimataifa la uhamiaji IOM kwenye jimbo la Western Equatoria nchini Sudan Kusini wanaendelea kutoa huduma za matibabu kwa wakimbizi wa ndani ambao hawana njia yoyote ya kufika kwenye vituo vya afya.

Makundi hayo yamekuwa yakisafiri mwendo mrefu kwenye barabara mbovu kuwafikia wakimbizi hao kwenye maeneo yaliyo karibu na mipaka ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Jamhuri ya Afrika ya kati. Wakimbizi hao walikimbia makwao mwaka 2008 kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara ya waasi wa Lords Resistance Army LRA kutoka nchini Uganda dhidi ya vijiji vyao.