Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO kwenye jitihada za kuangamiza minyoo nchini Guinea

WHO kwenye jitihada za kuangamiza minyoo nchini Guinea

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa hata kama kumepigwa hatua kubwa ukosefu wa fedha umetatiza juhudi za kuuangamiza ugonjwa wa Guinea Worm nchini Guinea ugonjwa unaosabaisha ulemavu. Karibu visa 1800 viliripotiwa mwaka 2010 ikilinganishwa na visa milioni 3.5 wakati kulianza mpango wa kuuangamiza ugonjwa huo mwaka 1980.

WHO inasema kuwa bado kuna visa vya ugonjwa huo kwenye nchi nne barani Afrika zikiwemo Sudan Kusini, Mali , Chad na Ethiopia. Ugonjwa huu husababishwa kwa kunywa maji machafu. Daktari Dirk Angels kutoka WHO anasema kuwa hata kama hakuna dawa ya kutibu ugonjwa huu hatua rahisi zitakazochukuliwa na jamii ni muhimu kwa kuuangamiza ugonjwa wa Guinea- Worm.

(SAUTI YA DR DIRK ENGELS)