Dola trilioni 1.6 zitumikazo kila mwaka kwenye masuala ya kijeshi, zingeweza kuchochea maendeleo-UM

4 Oktoba 2011

Kiasi cha dola za kimarekani trilioni 1.6 kinachotumika kila mwaka kwa ajili ya kugharimia shughuli za kijeshi kingeweza kusaidia pakubwa kusukuma mbele maendeleo na kukabiliana na janga la umasiki.

Hayo ni kwa mujibu wa afisa mmoja wa Umoja wa Mataifa anayehusika masuala ya uondoshwaji wa silaha ambaye ameongeza kuwa kuna haja sasa kwa mataifa makubwa na yale machanga kupunguza matumizi makubwa kwenye sihala na masuala ya kijeshi.

Afisa huyo Sergio Duarte akizungumza kwenye mkutano maalumu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa kwa hivi sasa kunamwamko mkubwa toka kwa mashirika ya kiraia na serikali zikijiingiza kikamilifu ili ulimwengu unaondokana na silaha za kinuklia.

Amesema ni jambo la kushangaza kuona kwamba matumizi kwa ajili nya kugharimia masuala ya kijeshi duniani kote imeongezeka na kufikia kiasi cha dola trilioni 1.6 ili hali mipango mingine ya kimaendeleo kama ule mpango wa maendeleo ya mellenia ukikwama kusonga mbele kutokana na kukosa vyanzo vya rasilimali.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter