Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchumi wa kimataifa usiokumbatia uzembe unahitajika(GA 66)

Uchumi wa kimataifa usiokumbatia uzembe unahitajika(GA 66)

Serikali kote duniani zimetakiwa kujitahidi kuchangia uchumi wa dunia ambao utaleta mustakhabali mzuri na sio kuwatunuku wasiojali. Wito huo umetolewa na Thomas Stelzer naibu katibu mkuu wa kamati ya pili inayohusika na masuala ya uchumi ambayo imeaanza kazi yake.

Bwana Stelzer amesema kuwa kukumbuka mwaka 2008 alipoanza mtafaruku wa chakula, nishati, uchumi na kuanguka kwa soko la fedha kuna haja ya kuchagiza dunia kujikita kwa kile alichokieleza kama masuala mazuri zaidi.

Amesema dunia inahitaji kufikiria mifumo mipya ya maendeleo, inahitaji mitazamo mipya ambayo itahakikisha uchumi unaendelea kukua, uhimili katika masala ya fedha, kuundwa kwa nafasi zaidi za kazi na njia ya moja kwa moja ya maendeleo endelevu. Dunia inahitaji uchumi utakaohimili vishindo na sio wa kuwafaidisha wachache.