Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watumiaji wa ardhi wasiojiweza lazima walindwe na sheria za kimataifa:UM

Watumiaji wa ardhi wasiojiweza lazima walindwe na sheria za kimataifa:UM

Haki za ardhi ni kikwazo cha kwanza katika kufikia lengo la usalama wa chakula, na bila kufikia muafaka wa kimataifa wa jinsi gani ardhi idhibitiwe basi haki za matumizi ya ardhi kwa watu wasiojiweza zitaendelea kuwekwa kando.

Onyo hilo limetolewa na mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa wa haki ya chakula Oliver De Schutter, ikiwa ni siku chache kabla ya majadiliano ya mwisho ya udhibiti wa ardhi yaliyoanza mjini Roma Italia. Bwana De Schutter amesema upokonyaji wa ardhi unakumbusha umuhimu wa kumiliki ardhi kwa kaya milioni 500 duniani zilizo na tatizo la chakula. Jason Nyakundi anaripoti.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)