Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ugonjwa wa kidingapopo waripotiwa Pakistan

Ugonjwa wa kidingapopo waripotiwa Pakistan

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa zaidi ya visa 12,000 vya ugonjwa wa kidingapopo vikiwemo vifo 125 vimeripotiwa nchini Pakistan hasa kwenye mkoa wa Punjab.

Msemaji wa WHO Tarek Jasarevic anasema kuwa WHO inayasaidia makundi yaliyobuniwa na serikali ya Pakistan kutoa hamasisho kwa umma. Pia amesema kuwa WHO imekuwa ikisaidia katika utoaji wa mafunzo kuhusu ugonjwa huo kwenye wilaya katika mikoa kadha. Mtaalamu wa ugonjwa huo kutoka WHO aliwasili nchini Pakistan juma lililopita kutoa mwongozo jinsi la kuuzuia ugonjwa huo.