Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban apongeza mafanikio ya mradi wa vijiji vya milenia

Ban apongeza mafanikio ya mradi wa vijiji vya milenia

Mafanikio ya mradi wa vijiji vya milenia ni mfano dhahiri kwamba kufikia malengo ya maendeleo ya milenia katika nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara sio tu inawezekana bali ni bayana. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo katika uzinduzi wa awamu ya pili ya mradi huo.

Ban amesema kwamba katika bara zima la Afrika ukuaji wa uchumi na uwekezaji binafsi vinasaidia kupunguza umasikini na kuboresha afya ya jamii. Amesema kuanzia mashinani sasa serikali zimeona umuhimu wa kuuimarisha mradi wa vijiji vya milenia.