Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukuaji wa miji ni lazima uzingatie mabadiliko ya hali ya hewa:Migiro

Ukuaji wa miji ni lazima uzingatie mabadiliko ya hali ya hewa:Migiro

Kuadhimisha siku ya kimataifa ya makazi duniani ujumbe umetolewa kwamba ukuaji wa miji unapaswa kuzingatia mabadiliko ya hali ya hewa.

Siku hii ambayo imetengwa na Umoja wa Mataifa kila Jumatatu ya kwanza ya mwezi Oktoba kauli mbiu ya mwaka huu ni “miji na mabadiliko ya hali ya hewa” lengo likiwa kutathimini hali ya miji na haki ya kila mtu kuwa na malazi katika miji hiyo, na kuikumbusha dunia wajibu wake wa kulinda makazi kwa mustakhabali wa maisha ya binadamu.

Akitoa ujumbe maalumu naibu Katibu Mkuu Asha-Rose Migiro amesema

(SAUTI YA ASHA ROSE MIGIRO)

Siku hii ya kimataifa ya makazi imeadhimishwa mijini Aguascalientes Mexico na hafla mbalimbali katika miji kote duniani.