Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nguvu ya pamoja ndiyo itayoweza kushida kasi ya madawa ya kulevya:UM

Nguvu ya pamoja ndiyo itayoweza kushida kasi ya madawa ya kulevya:UM

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na madawa ya kulevya na uhalifu ameonya kuwa hakuna njia ya mkato ambayo dunia inaweza kushinda vita ya usambazwaji wa madawa ya kulevya pasipo kuwepo kwa mashirikiano ya pamoja.

Akiwa ziara nchini Mexico, nchi ambayo inashudia wimbi kubwa la madawa ya kulevya, mkuu huyo Yury Fedotov amesema kuwa dunia inapaswa kuchukua jukumu la pamoja kukabiliana na vitendo vya usambazwaji wa madawa ya kulevya na kuongeza kuwa lazima hatua hizo zizingatie utashi wa pamoja.

Nchi ya Mexico iliyoko Kusin mwa Amerika inashika nafasi za usoni kwenye usambazaji na utumiaji wa madawa ya kulevya na ripoti za hivi karibuni zinaonyesha kuwa maeflu ya watu wameuwawa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kutoka na mikasa hiyo hiyo ya madawa ya kulevya

Rais wa nchi hiyo Felipe Calderón ambaye amekutana na mwenyeji wake, amehaidi kuendelea kufanya kazi na jumuiyaa za kimataifa ili kupunguza kitisho hicho.