Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukosefu wa fedha wasababisha kuzorota kwa hali kwenye kambi nchini Haiti

Ukosefu wa fedha wasababisha kuzorota kwa hali kwenye kambi nchini Haiti

Mratibu wa masuala ya kibinadamu kwenye Umoja wa Matifa Bi Valerie Amos amesema kuwa mengi ya mahitaji ya raia wa Haiti waliochwa bila makao kufuatia tetemeko kubwa la ardhi hayajatekelezwa kutokana na ukosefu wa fedha.

Karibu watu 600,000 bado wanaishi kwenye kambi tangu kutokea kwa tetemeko hilo mwezi Januari mwaka 2010 lililoharibu kisiwa hicho cha Caribbean. Kwa sasa wahisani wanaomba kuchangia hadi asimia 50 ya ombi la dola milioni 382 lilitolewana UM kwa taifa la Haiti.