Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe wa UM ataka kufanyika kwa uchaguzi wa amani nchini Liberia

Mjumbe wa UM ataka kufanyika kwa uchaguzi wa amani nchini Liberia

Afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia amewashauri raia wa nchi hiyo kuwa watulivu na kupiga kura kwa amani wakati Liberia inapojiandaa kwa uchaguzi wa Urais na wa Ubunge.

Ellen Margrethe Loj mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia ametoa wito kwa viongozi wa kisiasa wasichochee ghasia na pia akawataka wakubali matokeo ya kura hizo. Monica Morara na taarifa kamili.

(SAUTI YA MONICA MORARA)