Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maelfu ya wakimbizi wa ndani nchini Ivory Coast wahitaji makao ya dharura

Maelfu ya wakimbizi wa ndani nchini Ivory Coast wahitaji makao ya dharura

Maelfu ya wakimbizi wa ndani magharibi na kusini mashariki mwa Ivory Coast wanaoishi katika hali mbaya ya umaskini kwa sasa wanahitaji  makao ya dharura. Maeneo 14 walimokuwa wameweka kambi wakimbizi yamefungwa miezi michache iliyopita na kusababisha takriban familia 800 kubaki bila makao.

Maeneo mengine 15 kwa sasa yanahifadhi familia 1250 na huenda yakaondolewa. Kwa sasa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM kwa sasa linasimamia kambi 10 katika maeneo ya Guiglo na Duekoue zilizo makao ya wakimbizi wa ndani 17,100 ambao ni asilimia 66 ya wakimbizi wote. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)