Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM washutumu hukumu za wahudumu wa afya Bahrain

UM washutumu hukumu za wahudumu wa afya Bahrain

Taifa la Bahrain limeshutumiwa kwa kuwafunga wahudumu wa afya kwa misingi kuwa waliwahudumia waandamanaji waliokuwa wamejeruhiwa. Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa kuwa hukumu zilizotolewa kwa madaktari hao na raia wengine 34 si za ukweli.

Kati ya hukumu zilizotolewa na mahakama ya usalama wa kitaifa nchini Bahrain ni kati ya miaka mitatu hadi hukumu ya kifo. Rupert Colville kutoka ofisi ya haki za binadamu ya UM anasema kuwa hukumu hizo zinatia wasiwasi kwa kuwa ziliendeshwa kwenye mahakama ya kijeshi na washtakiwa hawakupewa nafasi ya kuwa mawakili.

“Wakili mmoja anayewakilisha wahudumu kadha wa afya aliwaambia waandishi habari kuwa hukumu hizo hazikudumu kwa zaidi ya dakika kumi, kati ya mashtaka ni pamoja na kukusanyika kinyume na sheria au kuonyesha chuki dhidi ya serikali , mauaji na uhalifu wa mali. Tunatoa wito kwa serikali kuhakikisha kuwa kila mmoja anayezuiliwa amehukumiwa kwa njia iliyo ya ukweli na amepewa muda wa kumtafuta wakili. Serikali imesema kuwa kesi zote zitapelekwa kwenye mahakama ya kiraia mwezi Oktoba na tunakaribisha tangazo hili, lakaini haibainiki jinsi rufaa za waliohukumiwa kwenye mahakama za kijeshi zitakavyoshughulikuwa kwenye mahakama za kiraia.”