Siku ya kimataifa ya wazee yaadhimishwa

30 Septemba 2011

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayehusika na haki ya kuwa na afya Anand Grover amesema kuwa watu wazee wana haki kama yeyote yule na ni lazima wapewe haki zao.

Akiongea wakati ya kuadhimishwa kwa siku ya kimataifa ya watu wazee Grover amesema kuwa mara nyingi watu wazee huwa wanapuuzwa na kunyimwa haki zao. Inakadiriwa kuwa watu milioni 700 duniani kwa sasa wana umri wa miaka sitini huku nchi zinazeondelea ndizo zinatarajiwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya watu wazee. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter