Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO na washirika wake waanzisha kampeni ya ugonjwa wa moyo

WHO na washirika wake waanzisha kampeni ya ugonjwa wa moyo

Mashirika ya kimataifaa yameanzisha kampeni maalumu kuelekea kwenye kelele cha maadhimisho ya kimataifa ya siku ya ugonjwa wa moyo ugonjwa ambao hupoteza maisha ya watu zaidi ya milioni 17 kila mwaka. Shirika la afya ulimwenguni WHO pamoja na lile linalohusika na moyo yameanza kampeni kuhamasisha nchi zaidi ya 100 juu ya tishio la ugonjwa huo na kuelezea sababu zinafanya watu kuangukia kwenye magonjwa ya moyo.

Katika kampeni hiyo shabaya kubwa inayotiliwa uzito na kuanisha maeneo ambayo yanaweza kumsababisha mtu kukumbwa na ugonjwa huo sababu ambazo zinatajwa ni pamoja kwa mtu kuwa na uzito kushinda mwili wake, ulaji wa chakula usiozingatia maelekezo ya kitaalamu pamoja na kukosa mazoezi ya viongo. Njia kuu inayotumiwa kwenye kampeni hii ni pamoja na kuendesha midahalao ha hadharani, mikutana kwenye maeneo ya wazo na njia ya maswali na majibu.