UM wasifu juhudi ya Colombia ya kupambana na madawa ya kulevya

29 Septemba 2011

Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na madawa na uhalifu UNODC ameipongeza Colombia kwa hatua inazochukua kupambana na uzalishaji wa madawa ya kulevya na uhalifu na pia kwa msaada wa fedha za kusaidia kutatua tatizo hilo katika eneo zima.

Mkurugenzi Mtendaji wa UNODC,Yury Fedotov, amemushukuru Rais Juan Manuel Santos kwa ukarimu wa mchango wa serikali yake kuwezesha mipango ya UNODC.

Colombia ambayo ni kiongozi wa ulimwengu katika uzakishaji wa koka, imeweza kupunguza kilimo cha mali ghafi ya cocaine kwa kiasi kikubwa katika muongo uliopita. Pia ukuaji wake wa kiuchumi umeonyesha wazi uwiano kati ya usalama wa taifa na kupunguka kwa ongezeko la madawa ya kulevya.

Bw Fedotov amesema maendeleo ya Colombia katika kupunguza uzalishaji wa madawa ya kulevya umekuwa wa dhahiri kimataifa katika suala la usalama na afya ya umma. UNODC iko tayari kuendelea kusaidia Colombia katika kukabiliana na changamoto zilizopo na zijazo kuhusiana na madawa ya kulevya na uhalifu.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter