Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hakuna njia ya suluhu la siasa nchini Afghanistan:UM

Hakuna njia ya suluhu la siasa nchini Afghanistan:UM

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan Staffan de Mistura amesema kuwa hakuna suluhu nyingine kwa siasa nchini Afghanistan. De Mistura ameyasema haya alipohutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hii leo kuhusu hali nchini Afghanistan.

Mjumbe huyo amesisitiza umuhimu wa watu wa Afghanistan wa kuendelea na jitihada za kutafuta amani hata baada ya kuuwa kwa mmoja wa wale waliokuwa wakiongoza mazungumzo baina ya wananchi wa Afghanistan Professor Burhanuddin Rabbani.

(SAUTI YA STAFFAN DE MISTURA)

Aghanistan inasaidiwa na kikosi cha kimataifa kinachoongozwa na jumuiya ya nchi za Magharibi NATO kuiwesesha Afghanistan kujenga vikosi vyake inapopambana na wanamgambo wa Taliban.