Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Haki za Binadamu la UM lataka Libya kurejeshewa uanachama wake

Baraza la Haki za Binadamu la UM lataka Libya kurejeshewa uanachama wake

Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa linataka uamuzi wa kutimuliwa kwa Libya kutoka uanachama wa baraza hilo kuondolewa. Libya ilitimuliwa kutoka kwa baraza hilo mwezi Februari mwaka huu kutokana na njia ilivyokabiliana na maandamano ya waliopinga utawala wa rais Muamar Gadaffi.

Wanachama wa baraza hilo walikaribisha yanayofanywa na baraza la kitaifa la mpito wa kulinda haki za binadamu, demokrasia na sheria. Baraza la kitaifa la mpito limeahidi kushirikiana na mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu ikiwemo ofisi ya tume ya haki za binadamu ya UM na tume ya kimataifa ya uchunguzi ya kuchunguza ukiukaji wa haki za binadamu nchini Libya.