Mahakama ya ICTR yathibitisha mashataka dhidi ya Warwanda wawili

29 Septemba 2011

Upande wa rufaa kwenye mahakama ya Umoja wa Mataifa kuhusu Rwanda hii leo umekiri mashtaka dhidi ya luteni Kanali Ephrem Setako na Yusuf Munyakazi ambaye alikuwa mkulima kwa kuhusika kwenye mauaji ya halaiki ya mwaka 1994 nchini Rwanda.

Setako na Munyakazi walihukumiwa kifungo cha miaka 25 tarehe 25 mwezi Februari na Juni 30 mwaka 2010. Upande wa rufaa ulitupilia mbali rufaa ya kanali Setako na kusema kuwa aliamrisha mauaji ya Watusi mwaka 1994 kwenye kambi ya Mukamira.

Naye Bwana Munyakazi anakabiliwa na mashataka ya kuhusuka kwenye mauaji ya Watutsi kwenye maeneo ya Shangi na Mibilizi mwaka 1994.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud