Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu 750,000 kwenye hatari ya kufa njaa nchini Somalia

Watu 750,000 kwenye hatari ya kufa njaa nchini Somalia

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya haki za binadamu kwenye pembe ya Afrika amesema kuwa watu 750,000 wako kwenye hatari ya kufa njaa nchini Somalia.

Shamsul Bari aliliambia Baraza la Haki za binadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva kwamba hali ya njaa nchini Somalia inazidi kuwa mbaya tangu atoe ripoti yake ya kwanza majuma sita yaliyopita. Amesema kuwa athari na ukame, njaa pamoja na mzozo uliopo vimesababisha madhara makubwa kwa maisha ya wasomali.

(SAUTI YA SHAMSUL BARI)