Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya kimataifa ya masuala ya bahari yaadhimishwa

Siku ya kimataifa ya masuala ya bahari yaadhimishwa

Umoja wa Mataifa umeadhimisha siku ya mabaharia duniani hii leo huku onyo likitolewa kwa gharama zinazopanda kutokana na kuongezeka kwa uharamia na wito kutolewa kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa, Serikali na wanajeshi kukabiliana na tatizo hilo.

Katibu Mkuu wa Shirika la kimataifa la Mababaria IMO Efthimios E. Mitropoulos anasema kuwa mabaharia 4, 185 walishambuliwa na maharamia mwaka 2010 , 1090 wakashikwa mateka na 516 wakatumika kama kinga. Alice Kariuki anaripoti.

(SAUTI YA ALICE KARIUKI)