Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sudan Kusini yaanza kupata ufadhili kutoka UM kwa ajili ya kukabili ukatili kwa wanawake

Sudan Kusini yaanza kupata ufadhili kutoka UM kwa ajili ya kukabili ukatili kwa wanawake

Taifa la Sudan Kusini lililozaliwa hivi karibuni hatimaye  limekuwa miongoni mwa mataifa 34 yaliyopewa ufadhili wa fedha na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kutekeleza miradi yenye shabaha ya kutokomeza vitendo vya unyanyasaji dhidi ya wanawake.

Iraq pia imeingia kwa mara ya kwanza kwenye kapu hilo ikipokea kiasi kadhaa cha fedha kwa shabaha hiyo hiyo moja. Kwa mujibu wa Bi Michelle Bachelet, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachohusika na masuala ya watoto, vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake ni mada muhimu inayopaswa kupewa msukumo wa pekee.

Mafungu hayo ya fedha yaliyotolewa yanatazamiwa kusaidia miradi mbalimbali yenye shabaha ya kukabiliana na wimbi la unyanyasaji dhidi ya wanawake.