Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ombi la utawala wa Palestina kujadiliwa na Baraza la Usalama la UM

Ombi la utawala wa Palestina kujadiliwa na Baraza la Usalama la UM

Mkuu wa masuala ya kisiasa kwenye Umoja wa Mataifa amesema kuwa utawala wa Palestina una uwezo wa kuwa taifa. Bwana Lynn Pascoe amesema haya alipohutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu hali kwenye eneo la mashariki ya kati.

Ombi lililotolewa na utawala wa Palestina la kutaka kuwa mwanachama kamili wa Umoja wa Mataifa limejadiliwa rasmi hii leo na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Rais wa Palestina Mahmoud Abbas aliwasilisha ombi hilo mbele ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon Ijumaa iliyopita. Mwangalizi wa Palestina kwenye Umoja wa Mataifa Riyad Mansour anasema kuwa Baraza la Usalama lilichukua maamuzi mawili wakati wa mkutano wake hii leo.

(SAUTI YA BWANA MANSOUR)

Bwana Mansour amesema kuwa mabalozi 15 ikiwemo kamati watakutana Ijumaa kuanza mpango wa kujadili ombi hilo.

Hata hivyo Marekani imesema kuwa itatumia kura ya turufu kwenye baraza la usalama la Umoja wa mataifa kuzuia ombi hilo