Wanachama wa UM wazungumzia masuala ya kimataifa kwenye baraza kuu la UM

28 Septemba 2011

Maafisa kutoka nchi wanachama wa Umoja wa mataifa wamefanya mijadala kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambapo wamezungumzia masula kadha yakiwemo mabadiliko ya hali ya hewa, maendeleo, na kumaliza ukwepaji wa sheria. Akihutubia mjadala huo balozi Lucy Mungoma kutoka Zambia amesema kuwa ghasia za kisiasa kaskazini mwa Afrika na mashariki ya kati zimeonyesha umuhimu wa majadiliano katika kusuluhisha mizozo.

Akikaribisha hatua za walibya za kumng’oa uongozi wa rais Muammar Qadhafi mapema mwaka huu hata hivyo bi Mungoma amesema kuwa uovu umetendwa dhidi ya watu weusi na wahamiaji kutoka nchi zingine za kiafrika.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter