Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aitaka Myanmar kufanya mabadiliko

Ban aitaka Myanmar kufanya mabadiliko

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema kuwa maendelo ya hivi majuzi yanaashiria kupigwa kwa hatua nchini Myanmar ambapo pia ameitaka serikali ya nchi hiyo kuhakikisha kuwa imefanya mabadiliko. Serikali mpya ilibuniwa kwenye taifa hilo la kusini mashariki mwa Asia miezi sita iliyopita ambapo rais Thein Sein ameahidi kupiga hatua mbele.

Ban amesema kuwa kuna fursa nginyi na kuongeza kuwa serikali inahitaji kufanya jitihada katika kufanya mabadiliko. Naye waziri wa mambo ya kigeni nchini Mynmar amesema kuwa serikali yake imezindua mzururu wa mabadiliko yakiwemo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii yaliyo na nia ya kuboresha maslahi ya watu wake.