Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAIDS yaipongeza Afrika Kusini kwa vita vyake dhidi ya ukimwi

UNAIDS yaipongeza Afrika Kusini kwa vita vyake dhidi ya ukimwi

Afrika ya Kusini imeonyesha mtazamo wa uongozi katika vita dhidi ya ukimwi kwenye miaka ya karibuni amesema mkurugenzi mkuu wa shirika la umoja wa Mataifa linalohusika na ukimwi UNAIDs Michel Sidibe.

Bwana Sidibe ambaye yuko ziarani nchini Afrika ya Kusini Jumatano hii amesema katika kipindi kifupi kumekuwa na matokeo mazuri kwa watu ambayo yanaonekana nchi nzima. Katika ziara yake ya siku saba nchini humo atajikita katika juhdi za serikali za kutaka kumaliza maambukizi mapya ya HIV miongoni mwa watoto ifikapo 2015, huduma.