Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Macho ya dunia sasa yako Sudan Kusini:Hilde Johnson

Macho ya dunia sasa yako Sudan Kusini:Hilde Johnson

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini Hilde Johnson amempongeza Rais wa taifa hilo jipya Salva Kiir kwa hotuba yake ya kihistoria kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa akisema ulikuwa ujumbe muafaka kwa wakati muafaka.

Amesema kuwa ujumbe huo Rais Kiir umedhihirisha nia yake ya kuwa na amani na taifa jirani la Sudan Kaskazini na kuanzisha msingi imara wa taifa hilo jipya wenye kujumuisha pande zote kisiasa, kuwa na utawala bora, wazi na uwajibikaji.

Hata hivyo ameongeza kuwa jinsi serikali ya taifa hilo jipya itakavyomudu usalama kwenye jimbo la Jonglei na kwengineko, na mchakato wa utawala, uwazi, uwajibikaji na kulinda haki za binadamu itakuwa muhimu sana kwa taifa la Sudan Kusini kuheshimika kimataifa.