Ugaidi bado ni tishio kubwa duniani:Ban

28 Septemba 2011

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema ugaidi bado ni tishio kubwa la usalama na amani duniani. Akizungumza kwenye kamati maalumu ya kupambana na ugaidi ya Umoja wa Mataifa amesema miaka kumi iliyopita siku kama ya leo Baraza la Usalama lilichukua hatua kukabiliana na tishio hilo la ugaidi dhidi ya amani na usalama wa kimataifa kwa kupitisha azimio namba 1373 ambalo lilikuwa muhimu sana katika vita vya kimataifa vya ugaidi.

Amesema miaka mitano baadaye azimio hilo likawa ni mkakati wa kimataifa wa kupambana na ugaidi chini ya uongozi wa Umoja wa Mataifa na amefurahishwa na shirikiano uliopo duniani katika juhudi za kuvishinda vita hivyo. Hata hivyo amesema ugaidi bado upo na unaendelea kutishia amani na usalama.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Azimio namba 1373 lilipitishwa wiki mbili tu baada ya mashambulizi ya Al-Qaeida kwenye majengo ya World Trade Center mjini New York.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud