Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO na njia za kupunguza gesi ya Carbon

FAO na njia za kupunguza gesi ya Carbon

Kuwepo kwa maeneo makubwa yenye misitu ni hatua kubwa ya kupunguza hewa chafu na kupanda kwa joto duniani kulingana na njia iliyoanzishwa na shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO kwa ushirikiano na taasisi moja nchini China.

Kwa sasa misitu mingi imeharibiwa na ikiwa itarejeshwa tena itasaidia kupunguza gesi ya Carbon na pia kuzuia mabadiliko ya hali ya hewa. Hata hivyo moja ya changamoto zilizopo ni ukosefu wa njia ya kubaini kiwango cha gesi ya Carbon inayochukuliwa na miradi inayohusiana na kilimo.