Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yaomba msaada wa kuwasaidia wakimbizi kutoka Sudan

UNHCR yaomba msaada wa kuwasaidia wakimbizi kutoka Sudan

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR pamoja na washirika wake wametoa ombi la fedha za kusaidia wakimbizi wanaoingia magharibi mwa Ethiopia kutoka jimbo la Blue Nile nchini Sudan. Mashirika hayo yakiwemo UNHCR, UNICEF, WFP na IOM yametoa wito wa jumla ya dola milioni 18.

Tangu mwezi Septemba wakimbizi 25,000 wamekimbilia Ethiopia huku idadi yao ikitarajiwa kuongezeka wakati eneo la Blue Nile linapoendelea kushuhudia mapigano. Adrian Edward ni kutoka UNHCR.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARD)